Ingia / Jisajili

Tujongee Meza Yake

Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Alfred Ogombo

Umepakuliwa mara 566 | Umetazamwa mara 2,353

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Tujongee meza – yake Bwana (atualika) kwenye karamuye yenye uzima, tule mwiliwe na tunywe damu yake

1.Ndugu jitayarishe – kwa kumpokea Yesu

   Katika maumbo ya mkate – nayo divai

2.Karamu takatifu – aliyotuandalia

  Yatutia nguvu kutufikisha – uzima wa milele

3.Kwa upendo wa Yesu mkuu - katupa mwiliwe tule

   Na damuye tuinywe kwa kweli – yumo ndani yetu

4.Ee Yesu Wewe kweli – ni chakula cha roho

   Utupe shibe kwani we’ ndiwe – mchungaji wetu

5.Kwako twapata amani – watupa tumaini

   Raha kamili pia watupa – kweli watujali


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa