Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 732 | Umetazamwa mara 2,533
Download Nota Download MidiKanisa langu mimi nitalitumikia siku zote
Kwa kipaji cha kuimba nitamtumikia Bwana wangu
Nawe jiulize njia ipi ndugu yangu utalitumikia kanisa la
Bwana, maana sisi sote tuna wito
1.Mwenyezi Mungu atuita kwa huduma mbalimbali,
jichunguze na ufahamu wito wako
Wewe kiungo muhimu kwa kanisa
2.Inaridhisha nyoyo zetu tukitimiza wajibu,
wetu wajibu, kwa kanisa lake Bwana
Na nafsi zetu pia zinafurahi
3.Yatekeleze majukumu yako kwa wadhifa wako,
ambao umechaguliwa ndugu yangu
Ujitolee kwa nguvu zako zote
4.Mimi na nyumba yangu nitalitumikia kanisa,
la Bwana siku zote za maisha yangu
Kwa kanisa nitakuwa mwaminifu