Mtunzi: Dr. David S. Kacholi
> Mfahamu Zaidi Dr. David S. Kacholi
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. David S. Kacholi
Makundi Nyimbo: Mama Maria
Umepakiwa na: David Kacholi
Umepakuliwa mara 1,519 | Umetazamwa mara 4,248
Download Nota Download MidiKiitikio: Salamu Mama mzazi mtakatifu wa Mungu, uliyemzaa mfalme mwenye kutawala mbingu na dunia daima na milele x 2
Mashairi:
1. Salamu Mama Maria, umebarikiwa, kuliko wanawake wote na mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
2. Utuombee Maria, Sisi wanawako, utuombee kwa mwanao ili tupate kuyashinda majaribu yote.
3. Malkia wa Malaika, Malkia wa Amani, Malkia wa upendo utuombee kwa mwanao Yesu Kristu.