Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Kwaresma
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 416 | Umetazamwa mara 2,299
Download Nota Download MidiNi kosa gani ulolifanya, kustahili haya mateso uliyoyapitia
Natambua kuwa yote haya, Bwana wangu uliyakubali ili niwe huru
1.Si kosa lako, si kosa lako bali makosa yangu,
yamefanya Bwana uteswe hivyo
2.Umeonyesha, upendo mkuu ulionao kwangu,
ukastahimili dhihaka zote
3.Natafakari, nastaajabishwa kujitolea kwako,
ukawa kafara kwa dhambi zangu
4.Niache dhambi, lengo langu kuu Bwana nikurudie,
na mapenzi yako niyatimize