Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Moyo Mtakatifu wa Yesu
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 514 | Umetazamwa mara 2,720
Download Nota Download MidiMoyo wake Yesu Mkombozi wa dunia
(Moyo) mpendelevu wenye uvumilivu
(Moyo) wa Bwana Yesu hazina ya neema
(Nyumba) ya Mungu Baba mlango wa mbinguni
(Moyo) wa Bwana Yesu Mtakatifu
1.Moyo mpenzi wa Mkombozi, dhambi zetu utuhurumie
Moyo wa Yesu tuunganishe, moyo wa Yesu furaha yetu
2.Kwako tunapata tumaini, amani pia watujalia
Utufungulie moyo wako, daima ndani yako tukae
3.Moyo wa Yesu chombo cha haki, moyo wa Yesu uzima wetu
Hekalu takatifu la Mungu, hema la Yule Aliye juu