Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Misa
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 973 | Umetazamwa mara 3,024
Download Nota Download Midi1.Tusikilize neno la Bwana x2 tulitangaze ulimwenguni
Neno la Bwana ni la uzima x2 latuletea amani tele
Bwana atualika wakristu – tumejaliwa kulisikia
Kwa maneno na matendo yetu – tulihubiri dunia yote
2.Neno la Bwana mwanga njiani x2 latuongoza maishani mwetu
Neno la Bwana raha shidani x2 latufariji maishani mwetu
Na kwa imani tulipokee – neno la Bwana kweli laokoa
Tunyenyekee tulisikilize – neno la Bwana latutakasa
3.Roho wa Bwana juu yangu mimi x2 Roho wa Bwana ‘kaniteua
Rasmi niende kwao maskini x2 niwaletee habari njema
Wafungwa na wapate uhuru – amenituma niwatangazie
Vipofu nao macho yaone – amenituma niwafungulie
4.Roho wa Bwana juu yangu mimi x2 Roho wa Bwana ‘kaniteua
Amenituma niwakomboe x2 niwakomboe wanaoonewa
Amenituma niutangaze – niutangaze mwaka wa wokovu
’kaniteua niutangaze – niutangaze mwaka wa wokovu