Ingia / Jisajili

Bwana Anakuja Ii

Mtunzi: Conrad Mghanga
> Mfahamu Zaidi Conrad Mghanga
> Tazama Nyimbo nyingine za Conrad Mghanga

Makundi Nyimbo: Majilio

Umepakiwa na: Conrad Mghanga

Umepakuliwa mara 179 | Umetazamwa mara 679

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
BWANA ANAKUJA II Chorus: Bwana anakuja Bwana anakuja (Bwana) Bwana anakuja kwetu kutuokoa x2. 1.Tutayarishe mioyo, kwa ujio wake Bwana, ili tupate okoka, kwani yeye ndiye Kristu, Mwokozi wa ulimwengu, yeye atatuokoa. 2.Mizigo yote ya dhambi, na tuiweke pembeni, Bwana aingie kwetu, kwani yeye ndiye Kristu, Mwokozi wa ulimwengu, yeye atatuokoa. 3.Mliovunjika nyoyo, mkaribisheni sasa, mpate kufarijika, kwani yeye ndiye Kristu, Mwokozi wa ulimwengu, yeye atatuokoa. 4.Wagonjwa wote wa mwili, na wale pia wa roho, njooni kwake anaponya, kwani yeye ndiye Kristu, Mwokozi wa ulimwengu, yeye atatuokoa.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa