Ingia / Jisajili

Tukusanye Vipaji

Mtunzi: Wachira Sammy
> Mfahamu Zaidi Wachira Sammy
> Tazama Nyimbo nyingine za Wachira Sammy

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Samuel wachira

Umepakuliwa mara 751 | Umetazamwa mara 2,432

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Chorus: Tupeleke vipaji vyetu kwa Mungu wetu Atabariki vipaji
               Tukusanye mazao yetu twende tupeleke
               (eeeh ametujalia uhai na nguvu, nasi yatupasa twende tupeleke)x2
1a) Vipaji hivi Baba twakutolea, kazi ya mikono yetu uvibariki
   b) Mkate huu Baba pia divai, tunakutolea Baba uvipokee.
2a) Na fedha hizi Baba twakutolea, japo ni kidogo Baba uzipokee
   b) Mazao yetu Baba twakutolea, kazi ya mikono yetu uibariki
3a) Furaha yetu Baba twakutolea, na udhaifu wa mwili utubariki
   b) Matendo yetu Baba twakutolea, pia na mawazo Baba utubariki
4a) Juhudi zetu Baba bidii yetu, tunazikabidhi kwako uzibariki
   b) Uchungu wetu Baba na shida zetu, tunajikabidhi kwako utubariki
5a) Watoto wetu Baba wazazi wetu, tunakutolea Baba uwabariki
   b) Mashamba yetu Baba mifugo yetu, vyote mali yakoBaba uvibariki.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa