Mtunzi: Paschal Francis Mgassa
> Mfahamu Zaidi Paschal Francis Mgassa
> Tazama Nyimbo nyingine za Paschal Francis Mgassa
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Mgassa Paschal
Umepakuliwa mara 492 | Umetazamwa mara 1,556
Download Nota Download MidiTUMTOLEE VIPAJI
Twendeni sote kwa Bwana,tumtolee vipaji,
Tumtolee vipaji vipaji vya kushukuru,
Tutoe kwa ukarimu tumpe Muumba wetu,
Tutoe kwa ukarimu Bwana atatubariki.
1. Sadaka ya Abrahamu ilimpendeza Mungu, nasi tutoe kwa moyo, Bwana atatubariki.
2.Kuhani Melkisedeki alimtolea Mungu, sadaka iliyo safi ikampendeza Mungu.
3. Sadaka yake Abeli katoa mazao bora, nasi tutoe kwa moyo Bwana atatubariki.
4. Sadaka na sala zetu tukamtolee Mungu, tutoe kwa ukarimu Bwana atatubariki.