Maneno ya wimbo
1.A: Hiki ndicho chakula (hiki ndicho chakula) kishukacho toka mbinguni (kishukacho mbinguni) aulaye mwili wangu anao uzima wa milele
B: Yeye ajaye kwangu (yeye ajaye kwangu) hataona njaa kabisa (njaa- ka-bisa) mtu akila chakula hi-ki ataishi milele.
KIITIKIO
Twendeni kwa karamu Kristo atualika leo twendeni twe-ndeni tukampokee Mfalme wetu x2
2.A: Alaye mwili wangu (alaye mwili wangu) huyo hukaa ndani yangu (hukaa ndani yangu) nitamfufua siku (mfufua) nitamfufua siku ya mwisho
B: Awe-zaje Yesu (awe-zaje Yesu) kutupa sisi mwili wake (kutupa mwili wake) tumesadiki ya kuwa (ya- kuwa) Mtakatifu wa Mungu
3.A: Wewe una maneno (wewe una maneno) ya uzima wa- milele (uzima wa milele) Bwana tupe siku zote (siku zote) u-tupe cha-kula hiki
B: Mkate mtakatifu (mkate mtakatifu) chakula safi kwa roho zetu (safi kwa roho zetu) jongeeni kwa heshima (kwa heshima) tukam-pokee Mungu wetu
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu