Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 495 | Umetazamwa mara 2,249
Download Nota Download MidiBila shaka twaamini (Kristu) unakaa hapo altareni [(nia yangu) ni kukuheshimu na kukuabudu niridhike moyoni] x2
1.Nafsi yangu inafurahi, nikikuabudu, Yesu mwema,
mwili na damu yako – Bwana utulishe utunyweshe
2.Naye aulaye mwilio, na kunywa damuyo, siku zote,
hataiona njaa – wala kiu hataiona
3.Twakiri ya kuwa Wewe, ni sadaka yetu, ni sadaka,
ya kutupatanisha – sisi na Baba Mungu Mwenyezi
4.Twaamini wakaa nasi, mpaka kufa kwetu, heri yako,
tujalie tufike – hadi tufike nawe mbinguni