Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Kwaresma
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 457 | Umetazamwa mara 1,880
Download Nota Download MidiNinasikitika – kwa mateso Bwana uliyapitia, kwa ajili yangu mwenye dhambi (kwa ajili yangu mkosefu) nipate nipate wokovu
1.Nakuomba msamaha Bwana wangu
Mateso makali hayo kwa’jili yangu
Kwa’jili yangu mwenye dhambi, mwenye dhambi
2.Dhambi zangu zimekufanya uteswe
Msalabani umehangaika Mwokozi
Dunia nzima waokoa, waokoa
3.Umedhihirisha upendo wako kwangu
Kifo chako msalabani Bwana wangu
Kimenifanya kuwa huru, kuwa huru
4.Mwana Kondoo umechinjwa kama sadaka
Damu yako ndicho chanzo cha wokovu wangu
Ndicho chanzo cha wokovu wangu, wokovu wangu