Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Misa
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 681 | Umetazamwa mara 2,783
Download Nota Download Midi1.Ngao yangu ni neno – Ni neno lake Bwana,
ni neno la ushindi, ni neno la wokovu
Ni ushuhuda wangu – Ni neno lake Bwana,
neno nitalitaja, pembe zote za nchi
Tulihubiri neno, hili neno la Bwana x2
2.Neno la msamaha – Ni neno lake Bwana,
latutakasa sote, ni neno la uzima
Tuliamini neno – Ni neno lake Bwana,
neno latuahidi, uzima wa milele
Ni neno takatifu, hili neno la Bwana x2
3.Vipofu wanaona – Ni neno lake Bwana,
neno la uponyaji, neno la miujiza
Viwete watembea – Ni neno lake Bwana,
neno la uponyaji, neno la miujiza
Tulitukuze neno, hili neno la Bwana x2
4.Limejaa hekima – Ni neno lake Bwana,
neno hili la Yesu, mshauri wa’jabu
Linalo mafundisho – Ni neno lake Bwana,
’tuelekeza kwenye, njia iliyo haki
Tulisikize neno, hili neno la Bwana x2
5.Neno linatujia – Ni neno lake Bwana,
leo linatujia, ni neno la baraka
Linatutia nguvu – Ni neno lake Bwana,
tuwapo safarini, safari hii ya roho
Tulieneze neno, hili neno la Bwana x2
Tulihubiri neno, – Ni neno lake Bwana
Ni neno takatifu – Ni neno lake Bwana
Tulitukuze neno – Ni neno lake Bwana,
Tulisikize neno – Ni neno lake Bwana
Tulieneze neno – Ni neno lake Bwana x2