Ingia / Jisajili

Msiwe Na Wasiwasi

Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Alfred Ogombo

Umepakuliwa mara 805 | Umetazamwa mara 4,137

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Msiwe na wasiwasi mkisema mtakula nini, au mnywe nini, au mtavaa nini Baba yenu wa mbinguni, anafahamu kwamba mnahitaji hayo yote

1.Waangalieni ndege ndege wa angani, wao hawapandi wala,

   hawavuni au kuweka ghalani lakini Baba, yenu wa mbinguni,

   huwalisha huwalisha hao

2.Fikirini maua ya shambani yameavyo, hayafanyi kazi wala,

   hayasokoti Sulemani kwa fahari yake yote, hakuvikwa kama,

   mojawapo ya hayo maua

3.Lakini ikiwa Mungu anayavika hivi, majani ya kondeni,

   yaliyopo leo na kesho kesho hutupwa motoni, naam atawavika,

   ninyi hata vizuri zaidi

4.Lakini utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake na yote,

   mtaongezewa msiwe na wasiwasi juu ya kesho, kwa sababu kesho,

   itajisumbukia yenyewe


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa