Maneno ya wimbo
TUFUNGUE HAZINA
Nyanyukeni wote tupeleke (kwake Mungu) yale ametupa kama mazao yetu, kwa shangwe kubwa twende bila kusita tukampe yote aliyotubarikia. { Kwa mikono (na) tubebe kwa miguu tupeleke tukamkabidhi kwani ni haki yakeTukusanye kwa wingi yale mema alotupa tukajaze ghala yake tubarikiwe.} x2
1. Tupelekapo vipaji hivi kwa Mungu, tunajiwekea hazina, hazina kubwa, huko juu mbinguni, hivyo tujikaze tufungue hazina.
2. Mungu wetu kweli amesema kwa upole, nijaribuni enyi watu kwa kutoa nanyi mtaona, nitaachilia baraka kuwabariki.
3. Na watoto wetu Mungu uwapokee, kwenye mikono mikono yako ya heri, ukawatakase na kuwabariki katika maisha yao.
4. Kazi zetu Bwana zinatupa matunda, ya kifedha pia na mali nyinginezo, twakuomba Baba, ukayapokee kisha utubariki.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu