Maneno ya wimbo
KWA BWANA KUMEKAMILIKA
1. Neno moja nimemwomba x2 Mungu Mwenyezi
Nalo ndilo nalisaka x2 Daima milele
Nikae nyumbani mwake siku zote, nipate faraja maishani mwangu { (kwani)
baraka zake (ni) nyingi, uzima wake (ni) mwingi na neema zake ni yeye ametupa } x2
( Nikae nyumbani mwake siku zote nipate faraja maishani mwangu ) x2
2. Mimi ninakaza mwendo x2 Nisichelewe
Niende nikamwone Yesu x2 Nimshukuru
3. Njoni kwangu ninyi nyote x2 Na mizigo yenu
Mimi nitawapumzisha x2 Mkaishi huru
4. Shambani mwake ee Bwana x2 Mavuno ni mengi
Hivyo nitakwenda mimi x2 Nikayavune yote
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu