Maneno ya wimbo
                MTOLEE MUNGU
1.Sasa ndio wakati wa kutoa sadaka jitayarishe mkristu ukamtolee Bwana, kikubwa au kidogo kwake sio tatizo bora umtolee kwa moyo moyo safi 
Mtolee mali yako,mtolee kwa mapendo, mtolee huyu Mungu ndiye mpaji wako (Mungu), amekupa toa ndugu, amekupa toa dada, amekupa huyu Mungu ndiye mpaji wako x2
2.Uhai amekupa afya kakujalia nafasi yako sasa urudishe shukrani, kazini unaenda mshahara wapata sio bidii yako bali ni kwa neema 
3.Mvua inyeshapo mimea husitawi mavuno unapata ni kazi yake Mungu, wafanya biashara faida unapata sio bidii yako bali ni kwa neema
            
                                    
                Nyimbo nyingine za mtunzi huyu