Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 518 | Umetazamwa mara 2,373
Download Nota Download MidiBwana Yesu tunakuabudu tunakiri U katika Hostya
Vichwa vyetu tunaviinamisha, na magoti tunakupigia
Maumbo ya mkate na divai, umo ndani tunakuabudu
1.Mwili wako ni chakula kweli, damu yako ni kinywaji kweli –
Twasadiki U katika Hostya, umo ndani kweli twasadiki
2.Umetupa chakula cha mbingu, tukiula hatuoni njaa
Umetupa kinywaji cha mbingu, tukiinywa hatupati kiu
3.Maji ya ubavu wako Bwana, yatutakasa daima sisi –
Kweli tunapata msamaha, kwa makosa tunayoyatenda
4.Umo humo Bwana wetu Yesu, twakuabudu twakusujudu –
Tunaamini umungu wako, wajitokeza kwenye altare