Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Pentekoste
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 878 | Umetazamwa mara 3,073
Download Nota Download MidiUje kwetu ewe Roho Mtakatifu - Uje ewe Roho Mtakatifu na Mfariji x2
1.Roho mwenye hekima Roho wa shauri na nguvu – Uje Roho
Ewe mwanga wenye heri tujaze neema mioyoni – Uje Roho
2.U Mfariji mwema sana u rafiki wetu sote –
Wape heri ya milele wanaokutumaini –
3.Roho mwenye uchaji washa moto wa mapendo –
Bila nguvu yako Wewe binadamu hana kitu –
4.Ewe Roho wa Bwana kaa nasi tuelekeze –
Wewe ni mfano mwema nasi sote tuuige –
5.Uwe nasi siku zote tupe heri ya milele –
Tukutumikie Wewe leo kesho na milele –