Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Mwanzo
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 579 | Umetazamwa mara 2,286
Download Nota Download MidiLeo hii wakristu leo hii twendeni tumwabudu Bwana hekaluni
Ni siku ya Bwana na imetakaswa twendeni (na) twendeni – tumfanyie shangwe Mfalme wa dunia na pia mbinguni
Hekaluni mwake – tupate baraka zake Bwana Mungu njoni leo njoni na tumwabudu
1.Twende kwake Bwana ni Mungu wetu – Twende kwa heshima na tumwabudu
Twende kwake Bwana Mfalme wetu –
Twende kwake Bwana Mlinzi wetu –
2.Nyumbani mwa Bwana nyumba ya sala – Nafsi ifurahi katika Bwana
Kwa heshima twende tukamwabudu –
Tupate neema na msamaha –
3.Sisi ni kondoo wa malishoye – Anatujalia ni Baba yetu
Katufanya sisi tupate shibe –
Ndiye atupaye na afya njema –
4.Sifa na heshima ni vyake Mungu – Yeye Mungu wetu anastahili
Mbingu na dunia ni Mtawala –
Utukufu wote wake na enzi –