Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 782 | Umetazamwa mara 2,351
Download Nota Download Midi1.Mungu ameniteua nilihubiri,
ni wajibu wangu kulihubiri neno
Kwa mataifa mbali mbali mataifa,
neno na lipenye kote lipenye kote
Mafundisho ya Bwana ni ngao yangu mimi, ni wapo vitani, dhidi ya shetani
Mafundisho haya hakika ni taa yangu, kuangaza njia, ya kufuata mimi
2.Neno lake Bwana ndugu halibagui,
kwani sote tuko sawa mbele ya Mungu
Analotaka Bwana tunyenyekee,
Tumakinike na tulisikize neno
3.Neno lake Bwana limejaa msamaha,
tumaini la uzima sote twapata
Vile yatupasa kuishi maisha yetu,
Bibilia ndilo mwongozo kamili
4.Neno la hekima ndilo neno la Bwana,
neno la wokovu ndilo neno la Bwana
Neno la uponyaji ndilo neno la Bwana,
neno la uhuru ndilo neno la Bwana
5.Akina baba wote msikie neno,
akina mama wote msikie neno
Nao vijana wote msikie neno,
nanyi watoto wote msikie neno