Ingia / Jisajili

Kumbuka Umavumbi

Mtunzi: Respice Makoko
> Mfahamu Zaidi Respice Makoko
> Tazama Nyimbo nyingine za Respice Makoko

Makundi Nyimbo: Mazishi

Umepakiwa na: RESPICE MAKOKO

Umepakuliwa mara 3,033 | Umetazamwa mara 9,497

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

Ewe mwanadamu kumbuka umavumbi, na mavumbini utarudi.x2

MASHAIRI

  1. Mwanadamu kumbuka kuwa umavumbi  wewe na mavumbini siku moja utarudi.
  2. Ulitoka katika tumbo bila ya mavazi na mavumbini siku moja utarudi.
  3. Nasi pia inatupasa kukumbuka kuwa tutarudia mavumbini siku moja.
  4. Mwanadamu ungama  dhambi na ufanye toba na Mungu Baba atafuta dhambi zako.
  5. Mwanadamu kumbuka kuwa una siku chache ulizopewa kuwa hai duniani.
  6. Mwanadamu kumbuka kuwa u kama maua yachanuayo hatimaye hunyauka.
  7. Na tumwombe Mungu Mwenyezi awahurumie awasamehe walioko Toharani.
  8. Tumtukuze Mungu Baba pia Mungu Mwana  tumtukuze naye Roho Mtakatifu.
  9. Kama mwanzo sasa na siku zote na milele na milele na hata milele amina.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa