Maneno ya wimbo
SADAKA SAFI
1.Hayawi hayawi tuchangamkeni sasa wakati ndio huu wa kutimiza wajibu, tuyatafakari maisha yetu wapendwa, yeye ametujalia bure bila malipo Mungu..
Siku zote anatulinda pia kutuongoza, ingawa sisi wenye dhambi bado anatupenda (hivyo) tumtolee mapato kama shukrani zetu (kwani) yote mali yake tumtolee kwa moyo safi (tena) tukumbuke yeye ndiye mpaji wa uzima (wetu) tuweke nadhiri za sadaka zetu kwake.
2.Tunajivunia mema mengi toka kwake, kuhesabu haya yote katu hatuwezi, hatulalamiki bali tunashukuru tu, twafahamu kwamba anatuwazia mema Mungu..
3.Manabii wa kale walimtolea pia sadaka safi tena za kuteke-tezwa, basi nasi leo tuige mfano wao, tutoe zaka na dhabihu zetu kwake yeye Mungu…
4.Bwana anasema nijaribuni sasa, ondoeni hofu mkiisha nikabiidhi, vipaji vyenu na matoleo yenu, mimi nitawabariki siku zote Mungu…
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu