Ingia / Jisajili

PENDO LA AJABU

Mtunzi: Conrad Mghanga
> Mfahamu Zaidi Conrad Mghanga
> Tazama Nyimbo nyingine za Conrad Mghanga

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Conrad Mghanga

Umepakuliwa mara 560 | Umetazamwa mara 1,528

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
PENDO LA AJABU Bwana pendo gani wewe (ukanipa) kwa kunifilia mimi (msalabani) hilo pendo lako Bwana (la ajabu) nami ninasema asante, (kwani pendo lako Ewe Yesu) halihesabu mabaya, (siku zote linavumilia) tena halinung'uniki, (hata siwezi kulieleza) pendo lako la ajabu {(kwa) maneno yangu (mimi) siwezi kabisa (ku) eleza jinsi unavyonipenda x2} Basi ninaahidi Yesu (kukutumikia) mimi na familia yangu (sote kwa pamoja) Tutatangaza jina lako (ili watu wote) wakujue wewe mfalme. 1. Ulinikomboa kwa njia ya kifo pale msalabani, kwa uchungu mwingi, aibu aibu Bwana ulipata kwa sababu ya kunipenda mimi. 2. Maadui zangu wanashangaa sana kwa jinsi gani unavyonipenda, hakika we Bwana ni rafiki mwema wanipenda sa--na. 3. Ulipofufuka ulikamilisha uokovu wangu hapa duniani na pia mbinguni. 4. Yesu nakupenda we mpenzi wangu, umevumilia uovu wangu, Bwana penzi lako ni la ajabu mno halijui mabaya ladumu siku zote Bwana.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa