Ingia / Jisajili

Mfalme Wa Dunia Kazaliwa

Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo

Makundi Nyimbo: Noeli

Umepakiwa na: Alfred Ogombo

Umepakuliwa mara 788 | Umetazamwa mara 2,809

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Mfalme wa dunia kazaliwa (leo) twimbe sote twimbe sote (aleluya) twimbe sote

(aleluya) vigelegele na tuvipige, shangwe tele,

tukamlaki Mtoto Yesu (ndiye) Mfalme wa mbingu na dunia

1.Ni furaha kuu iliyoje, nyuso zetu zimejaa furaha,

   uwepo wake Mungu Mwana leo tumeushuhudia

2.Hii ni siku yenye heri kwetu, amani ya kweli imeshuka,

   imeshuka toka mbinguni sote tumeishuhudia

3.Tuliopofushwa kwa maovu, dhambi zetu japo ni nyekundu,

   zitang’ara kama theluji, amekuja kutukomboa

4.Aleluya aleluya twimbe, huku tukizipiga makofi,

   tupunge mikono yetu, wimbo mzuri tumwimbie


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa