Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Kwaresma
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 1,473 | Umetazamwa mara 5,760
Download Nota Download Midi1.Yesu baada ya kupigwa mijeledi,
wahukumiwa ufe naye Pilato,
hata bila ya dhambi lolote
2.Yesu waupokea huo mzito msalaba,
kwani ni kwa ajili ya dhambi zetu,
watujalia wokovu wako
3.Yesu waanguka chini ya msalaba,
kwa udhaifu tena ukasimama,
nasi tuinue toka dhambini
4.Yesu Mama yako Maria mwakutana,
kwa ’pendo kwako moyoni aumia,
nasi pia tuheshimu Mama yako
5.Yesu wasaidiwa kuubeba msalaba,
naye yule Simoni wa Kirene,
tufanye msaada kwa wenzetu
6.Yesu wapanguzwa uso na Veronika,
waacha picha yako juu ya kitambaa,
tujalie ushupavu kutenda mema
7.Yesu waanguka chini mara ya pili,
kwa ubaya wa njia na ulegevu,
’tu wenye dhambi turehemu tena
8.Yesu wanawake wajawa na huruma,
wakulilia nawe wawafundisha,
tujalie huo moyo wa huruma
9.Yesu waanguka sasa mara ya tatu,
umedhoofika sana kwa mateso,
tupe neema tukufuate mpaka kufa
10.Yesu wao askari wakuvua nguo,
iliyogandamana nayo madonda,
daima tuwe wafuasi wako
11.Yesu wasulibiwa kwenye msalaba,
kwa maumivu damu inamwagika,
tupe moyo tuvumilie mateso
12.Yesu unakufa pale msalabani juu,
watukomboa sisi toka dhambini,
nasi tusitumikie tena dhambi
13.Yesu mwilio washushwa toka msalaba,
wawekwa mikononi mwa Mama yako,
Mama Bikira Maria tupokee
14.Yesu mwilio unazikwa kaburini,
kwa ubatizo wetu pia twazikwa,
tupokee Bwana saa ya kufa kwetu
15.Yesu siku ya tatu unafufuka,
ukashinda mauti ulivyosema,
tufufuke nawe siku ya mwisho