Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Mwanzo
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 3,141 | Umetazamwa mara 8,887
Download Nota Download MidiNimeingia nyumbani mwa Bwana (kwa shangwe) kwa shangwe na vigelegele, najisikia furaha nikiwa hekaluni kumwabudu Mwenyezi
Jitihada na nguvu zangu zote (na nia) naelekeza kwako Bwana, na nafasi umenipa kujongea kwako nikuabudu Mwenyezi
1.Kweli leo ni siku yenye heri, nimekuja nikuabudu –
kukuabudu Bwana Mungu
Nimefanikiwa kuwa mmoja, wa wale wamekuja leo –
kukuabudu Bwana Mungu
2.Umemimina neema yako kwangu, mhitaji wa fadhili zako –
yote mema yatoka kwako
Nimekuja nitoe ushuhuda, ushuhuda kwa wema wako –
yote mema yatoka kwako
3.Nyumbani mwako kuna msamaha, kwako kuna baraka tele –
nimekuja nikuabudu
Kwako kuna amani na furaha, wako uso n’tautafuta –
nimekuja kukuabudu