Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 740 | Umetazamwa mara 2,746
Download Nota Download MidiHaya maisha ninayoyaishi (kweli) si kwa uwezo wangu mimi (wala) uzuri wangu, bali yamemmgharimu Mungu wema wake
Kulala na kuamka kwangu (Mungu) ndiye anayezitawala (mimi) uwezo sina, hata wa kujiongeza sekunde moja
1.Mimi si mwema kuliko wale, waloonja mauti mbele yangu,
ila kwa neema yako mimi naishi
2.Nakosa kuwa na utulivu, nastaajabu kwa wema wako kwangu,
mimi ni nini hata unikumbuke
3.Kwa kweli siwezi kuhesabu, yale yote uliyonitendea,
siku zote wazidi kunineemesha
4.Njia gani nitakushukuru, nikuabudu vipi Mungu wangu,
kabisa ninashindwa nkutukuzeje
5.Nani awezaye kusimama, mbele yako nani mwenye heshima,
sifa na utukufu ni zako Wewe