Maneno ya wimbo
MT. AGOSTINO
Sauti tamu zasikika hewani (sauti) nzuri tena za kupendeza ni zetu sisi waimbaji wana Agostino, tunajituma kwa nguvu na akili (kabisa) tena tumekwisha jiandaa madhumuni yetu kufikisha injili kwa wote, (kwa nyimbo) Tunamshukuru Mungu (kwa vipaji) kwa karama alizotupa (tunaamini) tunapohubiri kwa nyimbo twasali mara mbili (hakika) Kwa maombezi yake (somo wetu) mtakatifu Agositino (tumepata) nguvu ya kuhubiri injili duniani kote.
1.Kwa usimamizi wako ooh tumeimarika sana kwani talanta zetu twazitumia vyema, nyota yetu inang’aa kwa msaada wako.
2.Mafundisho yako wewe ooh pamoja na mahubiri yote hayo ulifanya kwa ajili ya Mungu, Mwombezi tusaidie tufuate nyayo zako.
3.Mtetezi wa imani ooh imani ya waumini bila hofu ulitangaza habari ya wokovu, somo tusaidie tulinde imani yetu.
4.Mwinjilisti na mwalimu ooh mwenye huruma na upendo kanuni zako na sheria ndiyo mwongozo wetu, mwalimu utuombee sisi wahuburi.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu