Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Watakatifu
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 1,856 | Umetazamwa mara 6,646
Download Nota Download MidiMtakatifu wetu Yosefu twashukuru twakupongeza (kwa ulinzio mwema pia) kwa maombezi yako we' kweli u baba yetu sisi
1.Twajivunia kuitwa wanao – mzazi Mtakatifu wa Mkombozi
(wetu Yesu) uliyejitolea kumlea na kumlinda
2.Tulinde tusimame imara – katika hii imani yetu
(tuwe sote) hodari kulieneza neno lake Yesu
3.Majaribu mengi twayapata – humu duniani tujalie
(kuishi mfano) bora tupate tuzo la milele mbinguni
4.Hamu yetu kubwa kufuata – mfano wa familia takatifu
(tusi-vutwe) na ya dunia yanayotutenga na Mungu
5.Tuache utengano tujenge – mapatano palipo mapendo
(Mungu yupo) tueneze neno tujenge kanisa lake
6.Kukupenda ni kumpenda Yesu – tuombee daima kwa Bwana Yesu
('situ-ache) Mtakatifu Yosefu tunakutumaini