Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Pentekoste
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 1,191 | Umetazamwa mara 5,096
Download Nota Download MidiUje Roho Mtakatifu uje Mfariji,
zienee nyoyo za waamini wako
Na wote uwatie mapendo yako
Roho Mtakatifu uje Roho uje
1.Roho wake Bwana ’kajaza dunia – Uje Roho Mtakatifu uje
Imeviunganisha viumbe vyote – Uje Roho …
Hujua maana ya kila sauti – Uje Roho …
2.Roho aliwafundisha watu wote –
Wote wakajazwa Roho Mtakatifu –
Wakasema matendo makuu ya Mungu –
3.Akaunganisha makabila mengi –
Pamoja wakakiri imani moja –
Wote wakamshangilia kwa furaha –