Mtunzi: Thomas G. Mwakimata
> Tazama Nyimbo nyingine za Thomas G. Mwakimata
Makundi Nyimbo: Zaburi | Kupaa kwa Bwana | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata
Umepakuliwa mara 2,011 | Umetazamwa mara 5,952
Download Nota Download MidiMungu amepaa kwa kelele za shangwe x 2, Aleluya amepaa, amepaa Bwana amepaa kwa sauti ya baragumu x 2.
Mashairi:
1. Enyi watu wote, pigeni makofi mpigieni Mungu kelele kwa sauti ya shangwe.
2. Kwa kuwa Bwana aliye juu mwenye kuogofya, ndiye Mfalme mkuu wa dunia yote.
3. Mwimbieni Mungu naam imbeni mwimbieni, mwimbieni Mfalme wetu imbeni mwimbieni Mungu wetu.
4. Maana Mungu ndiye Mfalme wa dunia yote, imbeni kwa akili, Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake Kitakatifu.