Ingia / Jisajili

Tumaini Langu

Mtunzi: Conrad Mghanga
> Mfahamu Zaidi Conrad Mghanga
> Tazama Nyimbo nyingine za Conrad Mghanga

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani | Tenzi za Kiswahili

Umepakiwa na: Conrad Mghanga

Umepakuliwa mara 189 | Umetazamwa mara 952

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
TUMAINI LANGU 1.Mungu Muumbaji wa mbingu na dunia, wewe muanzilishi wa maisha yangu, waniongoza kwenye milima hata mabonde, wewe kiongozi mwema (Bwa-na) nakuamini Bwana Nainua macho yangu natazama (huko juu) kwa Imani nakutolea sala yangu, natazamia kupata msaada wako (msaada) maana wewe ndiwe tumaini langu x2. 2.Changamoto nyingi zinazoniandamana, nakutegemea uwe faraja kwangu, kwako nitapata heri na neema yakutosha, hujapungukiwa kitu (Bwa-na) nakuamini Bwana 3.Usafiri wangu kazi ya mwanadamu, nakutegemea uwe dereva wangu, barabarani angani hata kwenye bahara, mwelekezi wangu mkuu (Bwa-na) nakuamini Bwana Watu wote mliovunjika mioyo (vunjika mioyo), ninyi nyote mnaokata (tamaa msichoke) tamaa leo kumbukeni Mungu wenu,mtafuteni siku zote, kumbukeni kiongozi wenu mwenyezi Mungu, Mayatima na wajane njooni kwake (njooni njooni kwake), wote mlio wanyonge karibieni leo (karibieni leo), kumbukeni Mungu wenu,mtafuteni siku zote, kumbukeni kiongozi wenu mwenyezi Mungu, Yeye tumaini tumaini letu tumaini tumaini Mungu atuajali tumaini letu, Tuseme tumaini tumaini letu tumaini tumaini Baba atupenda tumaini letu, Tuimbe tumaini tumaini letu tumaini tumaini Mungu atukinga tumaini letu.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa