Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 599 | Umetazamwa mara 3,391
Download Nota Download MidiEe Mungu wangu nakuomba unikumbuke, mimi kiumbe chako (kilicho) dhaifu na mnyonge,
Mungu nakusihi usinisahau mimi (Bwana) nakuomba unikumbuke
1.Maisha yangu ya mashaka, sina raha amani sina,
ee Mungu wangu kaa nasi usiende mbali nami
2.Nakulilia mchana kutwa, Mungu wangu unihifadhi,
unikinge kwayo mabaya, Bwana wangu Mlinzi wangu
3.Ninapitia matatizo, bado nakutumainia,
kamwe hutaniacha mimi, ee Mungu uniokoe
4.Magonjwa yananiandama, na mengine hayana tiba,
uponyaji watoka kwako, uniponye Mungu wangu