Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Moyo Mtakatifu wa Yesu
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 842 | Umetazamwa mara 2,924
Download Nota Download MidiSiku za maisha yangu duniani [siku zote (mimi) nitaimba (kweli) nitasifu (kwa) kinywa changu nitataja sifa za moyo wa Yesu] x2
1.Moyo wa Yesu mpendelevu Mwana wa Mungu
Moyo ulio chemchemi ya uzima wetu
2.Kwako nafsi zetu zinapata kutulia
Ikiwa tuko kwenye dhiki watufariji
3.Watujalia baraka na amani tele
Kwa fadhili zako nyingi kweli watupenda
4.Japo sisi ni wenye dhambi unatujali
Unatusamehe makosa tunayotenda
5.Daima mimi nitaimba nitalisifu
Nitazimiminia sifa huu moyo wa Yesu