Mtunzi: Elijah M Kilonzi
> Mfahamu Zaidi Elijah M Kilonzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Elijah M Kilonzi
Makundi Nyimbo: Ndoa
Umepakiwa na: ELIJAH Mulei
Umepakuliwa mara 916 | Umetazamwa mara 2,544
Download Nota Download MidiMwenzangu pokea pete; kutoka leo nimeamua uwe wangu wa maisha, nami najitoa kwako niwe wako maishani,
tuishi tukipendana na kusaidiana tumekuwa kitu kimoja; Sauti naipasa dunia isikie, toka leo ijue sina nafasi tena
1. Na leo tumeunganishwa jinsi Mungu aliunganisha wazazi Adamu na Hawa humo shambeni mwa Edeni
2. Naapa mbele yake Mungu mimi sitakuacha kamwe nyakati za shida, furaha wewe kweli wangu maisha
3. Walounganishwa na Mungu binadamu 'sitenganishe, ndugu ukitutenganisha wewe utahukumiwa
4. Ewe Bwana ninakuomba tuongoze maishani tusije tukaichafua pete ya harusi yetu