Ingia / Jisajili

Utamu wa Bwana

Mtunzi: Elijah M Kilonzi
> Mfahamu Zaidi Elijah M Kilonzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Elijah M Kilonzi

Makundi Nyimbo: Mwanzo | Ubatizo | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: ELIJAH Mulei

Umepakuliwa mara 448 | Umetazamwa mara 1,297

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Njooni, njoni watu wote, njooni kwake Bwana; wazee kwa vijana, wakubwa kwa wadogo, wamama wasichana, wababa wavulana, njooni uonjeni utamu wake Bwana, maisha ya furaha, furaha ya milele.

1. Makabila, nchi zote, bara zote njoni kwa Bwana, (njoni onjeni utamu wa kukaa ndani yake)x2

2. Mayatima na wajane, na walopoteza mabibi (njoni kwake na upweke wenu utaondolewa)x2

3. Wagonjwa na wote walio nazo shida mbalimbali (zileteni shida zote kwa Bwana zitatuliwe)x2

4. Na wale wote mliofungwa na nyororo za dhambi (zileteni kwake Bwana leo azikatekate)x2

5. Ni maisha ya furaha kweli, maisha ya kuridhisha (sote twende Bwana atualika tukayaonje)x2



Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa