Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 2,097 | Umetazamwa mara 4,863
Download Nota Download MidiTwakutolea sadaka yetu moja (wapo) ya vitu vingi ambavyo umetujalia kwa neema yako Bwana (na sasa) Twanyenyekea Bwana Mungu Mkuu uzipokee na uzibariki
1.Sadaka yetu, na ikupendeze, iwe shukrani
(yetu) kwa yale mema yote tupatayo kwako
2.Twakusihi, Mungu tuepushe, mabaya yote
(Wewe) tumaini letu na upokee na shida zetu
3.Sifa zote, ee Bwana pokea, hapa tulipo
(ume)-tufikisha kwa uwezo wako ulio mkuu
4.Mimi kiumbe, chako dhaifu, mwanga wako na
(uni)-ongoze na unipokee jinsi nilivyo Bwana
5.Maombi yangu, na yakufikie, nakutolea
(kwa we)-ma wako Mungu yatakase na uyabariki
6.N’ni cha thamani, nikupe Mungu? Sina mi’ ila
(kido)-go ninacho kwa moyo wangu wote nakutolea