Maneno ya wimbo
                1.	Hebu nipisheni wote, nawasihi nipisheni  x2
{Nihubiri neno njema, duniani kwa kuimba
Kwani kuimba ni sawa, na kusali mara mbili} x2
                  Hebu nipishe shetani; nikahubiri x2
                  Hasira nyingi unaleta-kusudi nisihubiri
                  Ubishi pia            “           “            “
                  Udaku pia            “           “            “  
                  Vikwazo vingi     “           “            “
                  Lakini nitahubiri.
2.	Roho mtakatifu shuka, niongoze nikiimba x2
{Niguse roho za wale, wasiomwamini Yesu
Kusudi wajiunge, na kundi la kondoo wake} x2
3.	Baba, mama hata ndugu , nawasihi nipisheni x2
{Nijulishe watu Yesu ndie njia, kweli, uzima
Wakifuata Bwana Yesu wataenda hadi mbinguni} x2
4.	Bibi na watoto wangu, nawasihi nipisheni x2
{Niimbe niburudishe wanaopenda mziki
Hivyo basi kwa kuimba nivute wengi kwa Bwana} x2
5.	Jamii na marafiki, nawasihi nipisheni x2
{Niimbe niwafariji wenye shida mbalimbali 
Pia niwakumbusheni Bwana huyaweza yote} x2
6.	Ee Bwana uwaongoze waimbaji duniani x2
{Kuimba kwao kuweze kueneza neno lako,
Kufariji, hata pia kuweze kuburudisha} x2
            
                                    
                Nyimbo nyingine za mtunzi huyu