Ingia / Jisajili

Sala Ya Familia

Mtunzi: Dr. David S. Kacholi
> Mfahamu Zaidi Dr. David S. Kacholi
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. David S. Kacholi

Makundi Nyimbo: Mwaka wa Familia (2014)

Umepakiwa na: David Kacholi

Umepakuliwa mara 836 | Umetazamwa mara 3,517

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

kiitikio: Ee Mungu mwenyezi uliye asili ya familia, tunakushukuru kwa zawadi hii nzuri x2. Twakuomba, uzibariki familia zetu Ee Mungu, twakuomba, uziongoze na uzilinde Mungu wetu, dhidi ya maadui na upotofu wote x2.

1. Ee Mungu umetupatia familia ili wanadamu tukutukuze, wewe katika kuiendeleza kazi ya uumbaji.

2. Ee Mungu umetaka familia iwe shule yetu ya imani, upendo na tumaini upendo na tumaini.

3. Ee Mungu uzifanye familia ziwe chemichemi ya utakatifu, kwa kuwa watu wa sala na kushiriki sakramenti.

4. Ee Mungu zijalie familia moyo wa ukarimu na ujasiri, kupokea zawadi ya uhai mpya na kuutunza.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa