Mtunzi: James Muola Vavu
> Mfahamu Zaidi James Muola Vavu
> Tazama Nyimbo nyingine za James Muola Vavu
Makundi Nyimbo: Mama Maria
Umepakiwa na: James Vavu
Umepakuliwa mara 784 | Umetazamwa mara 3,895
Download Nota Download MidiSALAM MARIA
Bwana
yu nawe,
Umebarikiwa
kuliko wanawake wote;
Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
1. Imeandikwa kwamba,
Malaika Gabrieli akasema:
“Salam Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,
Umebarikiwa kuliko wanawake wote”
2. Imeandikwa kwamba,
Na yeye Elisabeti akasema:
“Na Yesu mzao, wa tumbo lako ‘mebarikiwa”
Mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
3. Imeandikwa kwamba,
Malaika ‘kampasha akasema:
“Siogope Maria, ‘mepata neema, ‘tamzaa mwana,
Mkuu jina Yesu mwana wa aliye juu”
4. Imeandikwa kwamba,
“Mwanamke ‘liyevikwa jua na mwezi
Na jua na mwezi, ulikuwa chini, ya miguu
yake,
Na juu ya kichwa chake nyota kumi na mbili.
5. Nasi tunakuomba,
Maria mtakatifu mama wa Mungu,
Mwombezi Maria, mama tuombee, ‘si wakosefu,
Sasa na saa ya kufa kwetu, Amina.