Ingia / Jisajili

Unilinde Ee Mungu

Mtunzi: James Muola Vavu
> Mfahamu Zaidi James Muola Vavu
> Tazama Nyimbo nyingine za James Muola Vavu

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: James Vavu

Umepakuliwa mara 217 | Umetazamwa mara 728

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Unilinde, unilinde, unilinde ee Mungu, Kwa maana nakimbilia kwako. 1. Bwana, ndiwe urithi wangu na kikombe changu, Ndiwe uishikiliaye hatima yangu. Nimemweka Bwana mbele ya macho yangu daima; Kwa kuwa yuko kulia kwangu, sitatikisika. 2. Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Roho yangu inashangilia mwili wangu utapumzika salama. Kwani hutaiacha nafsi yangu kuzimuni Wala hutakubali anayekuamini aone uharibifu. 3. Umenijulisha njia ya uzima Utimilifu wa furaha mbele ya uso wako, Na raha kulia kwako milele.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa