Mtunzi: Dr. David S. Kacholi
> Mfahamu Zaidi Dr. David S. Kacholi
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. David S. Kacholi
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito | Zaburi
Umepakiwa na: David Kacholi
Umepakuliwa mara 14,194 | Umetazamwa mara 23,804
Download Nota Download MidiKiitikio:
Tuongezee imani Bwana (tuongezee), tuongezee imani Bwana, tuongezee imani Bwana, tuongezee imani Bwana x 2
Mashairi:
1. Mitume kwa kutambua, uhitaji waliokuwa nao, hawakuona woga hawakuona woga wakuomba kuongezewa imani basi wakamwambia Bwana.
2. Inatupasa sisi wana wa taifa la Mungu, kutafakari kwa kina ile zawadi ya imani, iliyomiminwa ndani mwetu, hasa nyakati hizi zenye watu wengi wanaopata kigugumizi, cha kutambua na kukiri nguvu ya Bwana itendayo kazi ndani mwetu basi nasi tumwambie Bwana.
3. Na sisi kama mitume wa Yesu yatupasa kujipima imani tuliyonayo, na bila woga tumwombe Bwana Mungu tukisema.
4. Neno la Mungu ndio msingi wa imani yetu, Roho zetu zahitaji kulishwa kila siku na neno la Mungu, hivyo, nasi, tumwombe Bwana Mungu tukisema.