Ingia / Jisajili

Twende Tukaijenge Nyumba Ya Mungu

Mtunzi: Alexander M. Y. Kiyogera
> Mfahamu Zaidi Alexander M. Y. Kiyogera
> Tazama Nyimbo nyingine za Alexander M. Y. Kiyogera

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: MASHAKA YAKOBO

Umepakuliwa mara 285 | Umetazamwa mara 675

Download Nota
Maneno ya wimbo

Beti

1. Ee Mkristu jiulize, Ni mangapi umefanya kulijenga kanisa, pia ujifikirie ni vingapi umetoa kuligenga kanisa.

Kiitikio

Kumbuka kanisa ndiyo nyumba ya sala, ni nyumba ya Baba yetu, muumba wetu, mlishi wetu, hakika  ni nyumba ya Mungu.

Kujenga kanisa, ni kuweka hazina, mbingu patakatifu, kwake mwenyezi, penye salama hakika kwa mwokozi wetu.

Haya twende pamoja, kwa ukarimu, kwa moyo safi, kwa nguvu moja, simama, twende mbele za Bwana na fedha zetu tukaijenge nyumba ya Mungu.

2. Usikiapo tangazo, la ujenzi walalama na kulaum viongozi. Waleta vijisababu, Mara fedha zimekwisha uchumi umeporomoka.

3. Kanisa unalinyonya kwa huduma unazopta wewe ndugu hulijengi, wavuna usichopanda, kupewa zake huduma ikiwa wewe hujitoi.

4. Wajali mipango yako, wamuweka Mungu kando kwa kutojenga nyumba yake, Baraka akisifunga, kwako hutapata kitu, mipango yako itayumba.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa