Ingia / Jisajili

Enyi Viumbe Njoni Tusifu

Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Alfred Ogombo

Umepakuliwa mara 871 | Umetazamwa mara 3,200

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Enyi viumbe njoni tusifu na kuabudu mwili na damu [ya Yesu Kristu chakula na kinywaji cha uzima (mwili damu)] x2

1.Ametulisha kwa ngano bora – ametulisha kiini cha ngano

   Na ametushibisha asali – itokayo mbinguni

2.Bwana asema ndiye chakula – kilichoshuka toka mbinguni

   Mtu akila chakula hiki – ataishi milele

3.Mwili wake ni chakula kweli – damu yake kweli ni kinywaji

   Tukila mwili na kunywa damu – hatutakufa kamwe

4.Enyi binadamu wote njoni – njoni na tuinamishe vichwa

   Njoni tumwabudu Bwana Yesu – katika Ekaristi

5.Twakuabudu kifudifudi – twakuabudu na twakusifu

   U Mungu kweli na mwanadamu – katika Sakramenti


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa