Maneno ya wimbo
Bwana alitutendea mambo makuu;
Bwana alitutendea mambo makuu;
Tulikuwa tukifurahi, tulikuwa tukifurahi! x 2
1. Bwana alipowarudisha mateka wa Sioni,
Tulikuwa kama wanaoota ndoto.
Hapo kinywa chetu, kilijaa kicheko,
Na ulimi wetu, kelele za furaha.
2. Ndipo waliposema kati ya mataifa,
“Bwana amewatendea makuu.”
Bwana alitutendea mambo makuu,
Tulikuwa, tulikuwa tukifurahi!
3. Ee Bwana, uwarudishe wafungwa wetu,
Kama vijito huko Negebu.
Waliopanda kwa machozi watavuna
Kwa kelele, kelele za furaha.
4. Anayekwenda huku akilia,akichukua
Mbegu za kupanda, mbegu za kupanda.
Atarudi kwa kelele, kelele za furaha,
Akibeba, akibeba miganda yake.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu