Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 853 | Umetazamwa mara 2,920
Download Nota Download MidiJihadharini nao (mjihadhari na) manabii wa uongo (watu) wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo,
Walakini (kwa) ndani ni mbwa-mwitu wakali
Jihadharini na manabii manabii wa uongo
1.Mtawatambua kwa matunda yao x2 – Mtawatambua
kwa matunda kwa matunda yao
2.Je, watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika
mibaruti? - Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri,
Na mti mwovu (mti mwovu) – huzaa matunda mabaya
3.Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala
mti mwovu – kuzaa matunda mazuri, hauwezi
kuzaa matunda, matunda mazuri
4.Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa
motoni – Ndiposa kwa matunda (kwa matunda) yao
mtawatambua, kwa matunda yao mtawatambua