Ingia / Jisajili

Kwa Ajili Yetu

Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo

Makundi Nyimbo: Kwaresma

Umepakiwa na: Alfred Ogombo

Umepakuliwa mara 244 | Umetazamwa mara 1,058

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kwa ajili yetu Kristu akawa mtii,

Mpaka kufa, hata kufa msalabani

Mateso yako hayo mateso yako,

ni kwa’jili yetu, wenye dhambi

1.Pendo lako kwetu Bwana ni kuu,

   umechinjwa sadaka kwa’jili yetu

2.Yesu wangu mwema nihurumie,

   dhambi zangu zimesababisha hayo

3.Makali mateso umepitia,

   kunikomboa mimi mwenye dhambi

4.Ninakulilia ee Bwana wangu,

   kilio changu Bwana kikufikie

5.Bwana wangu Yesu uwasamehe,

   kwa kuwa hawajui walitendalo

6.Ukumbuke rehema zako Bwana,

   na huruma zako za tangu milele


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa