Ingia / Jisajili

Ee Mungu unirehemu

Mtunzi: Cpa M. B. Ngooh
> Mfahamu Zaidi Cpa M. B. Ngooh
> Tazama Nyimbo nyingine za Cpa M. B. Ngooh

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Zaburi

Umepakiwa na: Melkior Ngooh

Umepakuliwa mara 250 | Umetazamwa mara 1,323

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Mwanzo Dominika ya 26 Mwaka A
- Mwanzo Dominika ya 26 Mwaka B
- Mwanzo Dominika ya 26 Mwaka C
- Mwanzo Dominika ya 5 ya Kwaresma Mwaka C
- Katikati Dominika ya 24 Mwaka C
- Katikati Jumatano ya Majivu
- Katikati Dominika ya 1 ya Kwaresma Mwaka A
- Katikati Dominika ya 5 ya Kwaresma Mwaka B
- Katikati Dominika ya 3 ya Pasaka Mwaka C
- Shangilio Dominika ya 4 ya Kwaresma Mwaka C

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio

 

Ee Mungu unirehemu sawa sawa na fadhili zako, kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu X 2

 

Mashairi

 

1.     Unioshe kabisa na uovu wangu, unitakase Bwana unitakase dhambi zangu.

 

2.     Maana nimejua mimi nimejua makosa yangu, na dhambi yangu i mbele yangu daima.

 

3.     Nimekutenda dhambi wewe peke yako na kufanya maovu mbele za macho yako.

 

4.     Tazama naliumbwa katika hali ya uovu, mama yangu alinichukua mimba hatiani.

 

5.     Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, unioshe nitang’aa kuliko theluji.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa