Mtunzi: Cpa M. B. Ngooh
> Mfahamu Zaidi Cpa M. B. Ngooh
> Tazama Nyimbo nyingine za Cpa M. B. Ngooh
Makundi Nyimbo: Majilio | Mama Maria
Umepakiwa na: Melkior Ngooh
Umepakuliwa mara 1,566 | Umetazamwa mara 5,572
Download Nota Download MidiKiitikio
Malaika Gabriel
alitumwa na Mungu kwa Bikira Maria, akamwambia salama uliyepewa neema, Bwana yu
pamoja nawe. Tazama utachukua mimba na kumzaa mtoto mwanamume jina lake
utamwita Yesu X2
Mashairi
1. Malaika akamwambia usiogope Mariamu kwa maana umepata neema kwa
Mungu.
2. Mariamu akasema, mimi ni mjakazi wa Bwana na iwe kwangu kama
ulivyosema.
3. Malaika akamwambia, huyo atakuwa mkuu ataitwa mwana wa aliye juu.
4. Malaika akamwambia, Bwana
Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi Baba yake.
5. Malaika akamwambia, ataimiliki nyumba ya Yakob hata milele na ufalme
wake utakuwa hauna mwisho.